I'M TAZGENIUS MFALME WA DAWA TIBA ASILI TANZANIA

✨️
🖐Kila mtu ana kitu ambacho kinachochea kupata mafua akiwa nyumbani. Kwa wengine ni vumbi, marashi makali na wengine ni kuambukizwa na mtu mwenye mafua.
🖐Kwa mujibu wa tovuti ya Shirika la Mapafu la Marekani, mafua yanasababishwa na virusi vinavyoitwa influenza ambavyo huathiri koo, pua na mapafu.
🖐Shirika hilo limesema mafua yanaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu anayeumwa kupitia kuongea, kupiga chafya na hata kukohoa.
🖐Hata hivyo, zipo njia mbalimbali unazoweza kutumia mtu mzima kupambana na mafua awapo nyumbani kabla ya kwenda hospitali:
✨️Tumia maji ya uvuguvugu yenye tangawizi
🖐Tangawizi ni kati ya mizizi ambayo ina faida nyingi kiafya. Kwa mujibu ya tovuti ya masuala ya kiafya ya Healthline, kikombe cha maji ya moto yenye tangawizi kinaweza kumsaidia mtu kupooza mafua.
🖐Tangawizi pia inaweza kumsaidia mtu ambaye anakohoa au anayejisikia kichefu chefu.
💫Kunywa maji mengi
Kabla ya kufikiria kunywa dawa, huenda unayachukulia maji poa. Wasichokijua baadhi ya watu ni kuwa, endapo mwili ukiwa na maji itakusaidia kuondoa bakteria mwilini wakati ya kukohoa na kupiga chafya na ndiyo sababu ya watu wenye mafua kushauriwa kutokuzibana chafya zao.
Tovuti ya masuala ya lishe ya Nutritionnews inaeleza kuwa, mtu anayekunywa maji ya kutosha itamsaidia kukabiliana na vijimelea ikiwemo virusi kwa kuwa vitakuwa vinatoka hata kwa kupumua peke yake.
Endapo kunywa maji ni changamoto, unaweza kuangazia maji ya nazi, juisi, chai, matunda yenye maji na supu.