I'M TAZGENIUS MFALME WA DAWA TIBA ASILI TANZANIA
🇹🇿
Kiharusi husababishwa na nini?
Kiharusi husababishwa na kutokufika kwa damu sehemu ya ubongo.
Ikiwa mshipa wa damu unaopeleka damu kwenye sehemu ya ubongo ukaziba au kupasuka mtu yuko hatarini kupata kiharusi kama hajapata tiba haraka.
1.Kiharusi kinachotokea kwasababu mishipa ya damu kuziba husababishwa na mshipa wa damu kukamaa au kitu chochote kinachoweza kuziba mshipa.
Vitu vinavyoweza kuziba mshipa wa damu wa kwenye ubongo ni kama vile damu iliyoganda kwenye ubongo au sehemu ingine ya mwili na kusafiri mpaka kwenye ubongo.
Kiharusi kinachotokea kwasababu ya mshipa wa damu kuziba ndiyo aina ya kiharusi kinachotokea mara nyingi zaidi.
2. Kiharusi kinachotokea kwasababu sehemu ya mshipa wa damu kupasuka au damu kuvuja
Aina hii ya kiharusi husababishwa na vitu mbalimbali kama nilivyoviainisha hapa chini:
Kuwa na shinikizo la juu la damu: Shinikizo la damu linaweza kusababisha mishipa ya damu kwenye ubongo kusinyaa au kupasuka.
Mishipa ya damu inapopasuka au kukakamaa huongeza hatari ya sehemu za ubongo kukosa damu na kusababisha kiharusi.
Majeraha: Kuumia kwenye ajali moja kwa moja kwenye mshipa wa damu husababisha damu kuvuja na hivyo kutokufika kwenye sehemu ya ubonngo.
Dawa: Matumizi ya dawa zinzozuia damu kuganda yanahusishwa na kiharusi.
Magonjwa ya mishipa: Baadhi ya magonjwa ya mishipa mishipa kutanuka kunaweza kufanya mshipa wa damu kuvuja au kupasuka.
Dalili za kiharusi ni zipi?
Ubongo ni kiungo kinachoratibu shughuli zote za mwili na unawajibika kwa mawazo yetu yote, mienendo, na hisia.
Ubongo umegawanyika katika sehemu tofauti mbalimbali, kila sehemu ikiwajibika kwa kazi maalum.
Kwa mfano, sehemu yenye kudhibiti mienendo ya hiari kama kuongea, na sehemu zenye kushughulikia hisia kutoka kwenye sehemu mbalimbali za mwili.
Njia moja ya kuelewa kazi tofauti za ubongo ni kupitia picha ya ubongo ikionesha sehemu za ubongo zinazohudumia sehemu mbalimbali za mwili (Homonculus)
uwakilishi wa mwili wa mwanadamu katika ubongo, ambapo ufanyaji kazi wa kila kiungo cha mwili huakisi kiwango cha nafasi inayochukua kwenye ubongo.
Kwa mfano, mikono na mdomo vinawakilishwa kwa sehemu kubwa kuliko miguu na mgongo, kuonyesha ukubwa wa kazi ya mdomo katika kuhisi na wa mikono kufanya kazi.
Hivyo, shinikizo la damu linapoharibu mishipa ya damu katika ubongo, inaweza kusababisha dalili mbalimbali za mishipa ya fahamu, kulingana na eneo na ukubwa wa uharibifu.
Kwahiyo mgonjwa ataona dalili ambazo ni madhara ya kiharusi.
Madhara ya kiharusi
Madhara ya kiharusi kwenye sehemu ya ubongo husababisha mapungufu ambayo ndizo dalili za kiharusi. Madhara haya yanaweza kutofautiana lakini mara nyingi hujumuisha
Udhaifu wa ghafla au kufa ganzi upande mmoja wa mwili,
Ugumu wa kuzungumza au kuelewa mazungumzo,
Matatizo ya kuona, na
Kuhisi kizunguzungu au kutokuweza kusimama
Uso kwenda upande
Udhaifu kwenye mikono au miguu
Kichwa kuuma sana
Uangalizi wa kimatibabu wa haraka ni muhimu mtu anapopata kiharusi, kwani matibabu ya haraka yanaweza kusaidia kupunguza uharibifu wa ubongo na kuboresha matokeo ya tiba.