Meno Kulegea Na Hata Kung’oka Yenyewe. Ni watu wengi hasa wa kuanzia umri wa kati na kuendelea hupatwa na hali hii ya kuwa na meno yanayolegea na wanapoyachunguza hukuta meno husika hayana matundu na hali hii ya meno kulegea haiambatani na maumivu yeyote kwenye meno husika ama kinywani kwa ujumla wake. Kwa makundi mengine meno haya yaliyolegea huweza pia kung’oka kirahisi wanapong’atia kitu. Huu ni ugonjwa unaoathiri mfupa wa taya lililoshikilia meno husika, hivyo basi sehemu husika za mfupa wa taya ambazo hushikilia meno zinazoshambulia na ugonjwa huu huwa dhaifu na kipenyo chake kutanuka, mara kipenyo chake ambamo jino hujishika kinapotanuka jino husika huweza kulegea.

Kwa watu wengi wanapojichunguza meno yao huona kuna tabaka fulani gumu ambalo huwa limejijenga kwenye meno yao katika eneo ambalo jino hukutana na ufizi, kwa meno ya chini mara nyingi huwa ni kwa ndani ambapo meno hutazamana na ulimi lakini kwa meno ya juu tabaka hili gumu huweza kutokea pande zote. Kitaalamu tabaka hili gumu huitwa ugaga na huwa haiwezekani uwezi kuondoa ugaga kwa kupiga mswaki ama kwa kufanya flosi badala yake unahitajika kufanyiwa usafi kitaalam ili kuundoa.Kadiri tabaka laini na ugaga vinapokaa kwa muda mrefu kwenye meno yako, ndivyo hivyo huweza kuleta madhara. Mwanzoni huweza tu kufanya fizi zivimbe na kutoa damu unapopiga mswaki.
Mwendelezo wa fizi kuvimba hupelekea kutengeneza kwa nafasi katika meno yako ambazo pia hukaliwa na bakteria, tabaka laini na ugaga. Kadiri bakteria hawa wanapoendelea kuishi kwenye sehemu husika hutoa sumu ambayo huhusika moja kwa moja na kuendelea kwa ugonjwa huu. Kadiri muda unavyokwenda ndivyo nafasi hizi huzidi kukua na kufika mfupa ulioshikilia jino ambao nao unaposhambuliwa huwa dhaifu na kushindwa kuendelea kushikilia jino ambalo baadae hulegea na hata kung’oka.
Na pia kwa kalizia hii dawa itakusaidia kuondokana na harufu ya kinywa na kukufanya uwe safi muda wote.